728x90 AdSpace

  • Latest News

    Wednesday, September 23, 2015

    BALAA:FIFA KUBURUZWA MAHAKAMANI NA WALE MAKINDA WALIOIPONZA FC BARCELONA MPAKA IKAZUIWA KUSAJILI


    Unalikumbuka lile sakata la FIFA kuifungia FC Barcelona kwa kosa la kusajili wachezaji makinda waliochini ya miaka 18 tena kwa njia za panya na kukiuka kipengere cha 19?Sasa wale wakinda wanajipanga kuishtaki FIFA kwa madai kuwa inaua vipaji vyao.

    Hii ni kutokana na ukweli kwamba mbali ya FIFA kuifungia FC Barcelona kutofanya usajili wowote mpaka januari mwakani pia iliwapinga marufuku makinda hao 10 walio chini ya miaka 18 kutoichezea FC Barcelona,kutofanya mazoezi na kikosi cha kwanza na kutoendelea kuishi katika shule ya soka inayomilikiwa na klabu hiyo ya La Masia.

    Baadhi ya makinda  waliokumbwa na rungu hilo la FIFA ni kutoka Cameroon na Korea Kusini akiwemo kinda wenye vipaji kikubwa Lee Seung-Woo pamoja na wengine toka America,akiwemo Ben Lederman.

    Baba mzazi wa kinda Lederman aitwaye Danny,ambaye ni wakili wa California, amepanga kulifikisha shauri hilo katika mahakama ya michezo (CAS).Akiongea na gazeti la Mundo,Danny amesema "FIFA haiwezi kuamua maisha ya mtoto wangu.FIFA inajali pesa,kombe la dunia na faida tu.Watakwenda wapi watoto waliotoka Cameroon?Tunazunhumzia suala la haki za binadamu hapa.Najua kufika CAS ni gharama sana lakini hakuna jinsi lazima tufike huko.Nafanya hili kwa ajili ya watoto wengine walio katika hali kama ya mwanangu"
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: BALAA:FIFA KUBURUZWA MAHAKAMANI NA WALE MAKINDA WALIOIPONZA FC BARCELONA MPAKA IKAZUIWA KUSAJILI Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top