Hatimaye Mwenyekiti wa Yanga SC, Yussuf Manji amemaliza tofauti zake na kampuni ya Azam TV na kukubali klabu yake kusaini mikataba yote ya kampuni hiyo, mali ya Alhaj Sheikh Said Salim Awadh Bakhresa.
Habari kutoka ndani ya Yanga SC,zinasema kwamba klabu hiyo sasa inatarajiwa kusaini mkataba wa haki za Televisheni wa Azam FC na pia wa kipindi cha Yanga TV, ambayo kwa pamoja itawafanya wapokee si chini ya Sh. Milioni 600.
Mechi za Yanga SC zimekuwa zikionyeshwa kama kawaida na Azam TV, lakini kwa miaka yote miwili klabu haijachukua mgawo wake Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).
0 comments:
Post a Comment