London,England.
TOTTENHAM imetambulisha rasmi jezi zake mpya za msimu wa 2017-2018 tayari kwa kimuhemuhe cha michuano ya ligi kuu England na michuano ya klabu bingwa Ulaya.
Kwa mara ya kwanza katika historia itashuhudiwa Tottenham ikivaa jezi za NIKE baada ya kupata dili kubwa la Pauni Milioni 30 kutoka kwa kampuni hiyo yenye makao makuu yake nchini Marekani.
Awali Tottenham ilikuwa ikivaa jezi kutoka kampuni ya Under Armour ambayo safari hii imezidiwa ujanja na NIKE.Tottenham itaanza kuzitumia jezi hizo mpya Julai 22 mwaka huu pale itakaposhuka dimbani kuvaana na PSG.
0 comments:
Post a Comment