728x90 AdSpace

  • Latest News

    Saturday, July 01, 2017

    CHELSEA YAMNASA KIPA BABU WA MAN CITY

    London,England.

    MABINGWA watetezi wa taji la ligi kuu ya soka nchini England,Chelsea wameongeza sura mpya kikosini kwao baada ya hii leo kumsajili kipa wa zamani wa Manchester City,Willy Caballero.

    Caballero mwenye umri wa miaka 35 amejiunga na Chelsea kwa uhamisho huru baada ya kuachwa na Manchester City mwishoni mwa msimu uliopita.

    Chelsea imeamua kumsajili Caballero anayetokea Argentina ili kuchukua nafasi ya aliyekuwa kipa wake chaguo la pili,Asmir Begovic aliyejiunga na Bournemouth kwa dau la €8m.

    Caballero anakuwa mchezaji wa pili kujiunga na Chelsea katika siku hii ya leo.Mwingine ni kinda Ethan Ampadu,18, aliyetokea Exeter.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: CHELSEA YAMNASA KIPA BABU WA MAN CITY Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top