London, England.
EVERTON imeripotiwa kukamilisha usajili wa mshambuliaji hatari wa Malaga ya Hispania,Sandro Ramirez,21.
Kwa mujibu wa habari kutoka The Express,Everton imefanikiwa kumsajili mshambuliaji huyo wa zamani Barcelona licha ya kuwepo kwa taarifa kuwa Atletico Madrid ilijaribu kutibua dili hilo katika dakika za mwisho kwa kutaka kupanda dau.
Usajili huo ambao umeripotiwa pia na Sky Sports umedaiwa kuigharimu Everton kiasi cha £5.25m kumnasa mshambuliaji huyo aliyeifungia Malaga mabao 14 na kupika mengine matano katika michezo 30 ya ligi ya La Liga msimu uliopita.
Ramirez aliyejiunga na Malaga msimu uliopita baada ya kutupiwa virago na Barcelona amejiunga na Everton kwa mkataba wa miaka mitano na atakuwa akivalia jezi namba tisa (9).
Ramirez anakuwa mchezaji wa nne kujiunga na Everton katika kipindi hiki cha usajili barani Ulaya.Wengine ni Jordan Pickford, Davy Klaassen na Henry Onyekuru.
0 comments:
Post a Comment