Dar Es Salaam.
KIPA mahiri nchini, Deogratius Munishi ‘Dida’, msimu ujao hatakuwa sehemu ya kikosi cha mabingwa wa kihistoria wa ligi kuu bara,Yanga.Imebainika.
Hilo limebainishwa na kocha wa makipa wa Yanga,Juma Pondamali Mensah wakati akifanya mahojiano na kipindi cha michezo cha Sports Leo kinachorushwa na kituo cha Radio One cha jijini Dar Es Salaam.
Pondamali amesema wameamua kuachana na Dida baada ya kipa huyo wa zamani wa Simba na Azam kukataa kuongeza mkataba mpya akitaka asubiriwe mpaka hapo atakaporejea kutoka nchini Afrika Kusini anakotarajia kwenda kwa ajili ya majaribio.
Pondamali amekwenda mbali zaidi na kusema kuwa tayari Yanga imeshaziba pengo la Dida kwa kumsajili kipa Mcameroon wa African Lyon,Youthe Rostand ambaye kifundi ni mzuri sana kuliko makipa wa hapa nchini.
Kwa mujibu wa Pondamali ni kwamba msimu ujao Yanga itakuwa na makipa watatu ambao ni Youthe Rostand ,Beno Kakolanya pamoja na kipa mwingine mdogo ambaye hakutaka kumtaja jina.
0 comments:
Post a Comment