Moscow, Urusi.
IKICHEZA bila ya staa na nahodha wake,Cristiano Ronaldo,Ureno imetwaa nafasi ya tatu baada ya kufanikiwa kutoka nyuma na kuifunga Mexico mabao 2-1 katika mchezo mkali wa kusaka mshindi wa tatu uliochezwa jioni ya leo kwenye Uwanja wa ulioko huko Otkrytiye Arena Moscow, Urusi.
Mabao yaliyoipa ushindi huo Ureno yamefungwa na Pepe katika ya 91 na Adrien Silva kwa mkwaju wa penati katika dakika ya 104.Bao la Mexico limepatikana dakika ya 54 baada ya beki wa Ureno,Neto kujifunga akijaribu kuokoa hatari langoni mwake.
Aidha katika mchezo huo ilishuhudiwa Ureno na Mexico zikimaliza baada ya wachezaji wao wawili Miguel Layun na Nelson Semedo kutolewa nje kwa kadi nyekundu.
0 comments:
Post a Comment