Krakow, Poland.
UJERUMANI imetwaa ubingwa wa michuano ya Ulaya (Euro) kwa wachezaji walio na umri wa chini ya miaka 21 baada ya usiku wa kuamkia leo kuwafunga mabingwa wa kihistoria wa michuano hiyo Hispania kwa jumla ya bao 1-0 katika mchezo wa fainali uliochezwa huko Krakow, Poland.
Bao lililoipa Ujerumani ubingwa huo wa kwanza wa vijana tangu mwaka 2009 limefungwa kwa kichwa katika dakika ya 40 na kiungo Mitchell Weiser akiunganisha krosi safi kutoka kwa mlinzi wa kulia,Jeremy Toljan.
Wakati huohuo nahodha wa Hispania,Saul Niguez anayeichezea Atletico Madrid ameibuka mfungaji bora wa michuano hiyo baada ya kufunga mabao matano kwenye michuano hiyo.
0 comments:
Post a Comment