Dar Es Salaam,Tanzania.
Kamati ya Utendaji ya Shrikisho la Soka Tanzania (TFF) inatarajiwa kukutana kwa dharura kesho asubuhi kujadili mustakabali wa shirikisho hilo baada ya Rais wake Jamal Malinzi kuwekwa ndani kwa makosa ya kutakatisha fedha juzi Alhamisi.
Malinzi na Katibu Mkuu wa TFF, Mwesigwa walisomewa mashtaka 28 ikiwemo kutakatisha fedha na kughushi huku wakiwekwa ndani hadi Julai 3, kwa kukosa dhamana.
"Katika hili lililotokea tumeona tuitishe kikao cha kamati ya utendaji kesho ili kujadiliana kuhusu namna ya kufanya. Na bahati nzuri wenzetu wa Fifa wamenipigia kunihoji kuhusu hilo hivyo tunatarajia kuwa na kikao kingine Jumanne ambacho tutakuwa na wajumbe kutoka Fifa," alisema makamu wa Rais wa TFF, Wallace Karia.
Karia alisema kuwa mchakato wa uchaguzi utaendelea kama kawaida chini ya kamati ya uchaguzi.TANGAZA BIASHARA YAKO NASI
Simu : + 255 675 734 252
+ 255 717 705 548
Email : sokaextra82@gmail.com
0 comments:
Post a Comment