Kazan,Urusi.
MABINGWA ya,Ureno wameanza kinyonge kuusaka ubingwa wao wa kwanza wa kombe la mabara ambalo hushirikisha mabingwa kutoka mabara saba yanayoiunda dunia baada ya jioni ya leo kulazimishwa sare ya kufungana mabao 2-2 na mabingwa wa Amerika Kaskazini,Mexico katika mchezo wa kundi A uliochezwa kwenye uwanja wa Kazan Arena.
Ureno ndiyo waliokuwa wa kwanza kupata bao la kuongoza katika dakika ya 34 kupitia kwa Ricardo Quaresma.Quaresma alifunga bao hilo akimalizia pasi ya nahodha Cristiano Ronaldo aliyewazidi ujanja mabeki wawili wa Mexico na kutoa pasi kwa mfungaji.
Kuingia kwa bao hilo kuliwaamsha Mexico ambao walikuja juu na kufanikiwa kupata bao la kusawazisha katika dakika ya 42 kupitia kwa Javier Hernández "Chicharito" aliyefunga kwa kichwa akiunganisha pasi ya Carlos Vela na kufanya mchezo huo uende mapumziko ukiwa sare ya bao 1-1.
Kipindi cha walikuwa ni Ureno tena waliokuwa wa kwanza kupata bao la pili katika dakika ya 86 kupitia kwa beki wao wa kulia Cedric Soares.
Mchezo ukiwa unaelekea kumalizika Hector Moreno aliifungia Mexico bao la pili kwa kichwa katika dakika ya 91 akiunganisha kona iliyopigwa kutoka kushoto mwa uwanja na kufanya mchezo uishe kwa sare ya kufungana mabao 2-2.
Vikosi
Mexico:Guillermo Ochoa, Carlos Salcedo, Diego Reyes, Héctor Moreno,Miguel Layún, Andrés Guardado, Jonathan
Dos Santos, HĂ©ctor Herrera, Carlos Vela,Javier “Chicharito” Hernández y RaĂşl JimĂ©nez.
Ureno:Rui Patricio,CĂ©dric Soares, JosĂ© Miguel da Rocha Fonte, KĂ©pler Laverán Lima Ferreira,William Carvalho, Gelson Batalha, Joao Moutinho, AndrĂ©s Gomez, Cristiano Ronaldo y Luis Carlos Almeida “Nani”.
0 comments:
Post a Comment