Johannesburg,Afrika Kusini.
MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Zimbabwe, Donald Ngoma ameviacha kwenye mataa vilabu vya Simba na Yanga baada ya hii leo kujiunga na Polokwane City inayoshiriki ligi kuu nchini Afrika Kusini.
Ngoma mwenye umri wa miaka 27 amejiunga na Polokwane City kwa mkataba wa miaka mitatu baada ya kumaliza mkataba na mabingwa wa Tanzania, Yanga aliojiunga nao miaka miwili iliyopita akitokea FC Platinum ya nyumbani kwao Zimbabwe.
0 comments:
Post a Comment