Dar Es Salaam,Tanzania.
RAIS wa shirikisho la soka Tanzania,Jamal Malinzi pamoja na katibu wake mkuu Celestine Mwesigwa leo Alhamisi wamesomewa mashtaka 28 kwenye mahakama ya Kisutu jijini Dar Es Salaam baada ya jana kutiwa nguvuni na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kwa makosa ya rushwa pamoja na matumizi mabaya ya ofisi.
Baadhi ya makosa hayo ni pamoja na Kughushi waraka wa kamati ya utendaji ulioonyesha kuwa EXCOM imeridhia kubadilishwa kwa Signatories wa Bank hii inamhusu Malinzi na Mwesigwa pia,
Kufoji risiti za kuwa Malinzi anaidai TFF (risiti zipo zaidi 20 zinazodaiwa kufojiwa) hii inamhusu Malinzi pekee
Na Mwisho ni shitaka la kutakatisha fedha dola za kimarekani 375,418 hii inamhusu Malinzi, Mwesigwa na Nsian
Makosa hayo 28 yamewanyima haki ya kupata dhamana viongozi hao na badala yake wakataa rumande mpaka hapo Juni 13 ambapo kesi yao itasomwa tena.
0 comments:
Post a Comment