728x90 AdSpace

  • Latest News

    Thursday, June 29, 2017

    STARS DIMBANI TENA LEO SAUZI,IKISHINDA KUWAVAA WENYEJI ROBO FAINALI COSAFA CUP


    Rustenburg,Afrika Kusini.

    TIMU ya taifa ya Tanzania,Taifa Stars leo jioni mishale ya saa 12:00 za Tanzania itashuka dimbani huko Moruleng nchini Afrika Kusini kucheza na Ushelisheli katika mchezo wake wa mwisho wa kundi A wa michuano ya kombe la Cosafa.

    Taifa Stars ambayo iko kileleni mwa kundi A ikiwa na pointi nne kibindoni inaingia kwenye mchezo wa leo ikiwa na kumbukumbu nzuri ya kupata matokeo chanya katika michezo yake miwili ya awali huku ikitambua kuwa ushindi wowote mzuri dhidi ya Ushelisheli utaipa tiketi ya kutinga robo fainali ambapo itacheza na mwenyeji wa michuano hiyo Afrika Kusini.

    Taifa Stars inayonolewa na kocha mzawa,Salum Mayanga baada ya kuifunga Malawi mabao 2-0 katika mchezo wake wa kwanza kabla ya kutoka sare ya bila kufungana na Angola ambayo pia leo itashuka dimbani kucheza na Malawi huko Royal Bafokeng.

    Kama ilivyo kwa Taifa Stars,Angola nayo ina pointi nne ilizozipata baada ya kuifunga Ushelisheli bao 1-0 kabla ya kutoka sare ya bila kufungana na Taifa Stars.Timu zote mbili zina nafasi ya kutinga robo fainali.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: STARS DIMBANI TENA LEO SAUZI,IKISHINDA KUWAVAA WENYEJI ROBO FAINALI COSAFA CUP Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top