728x90 AdSpace

  • Latest News

    Wednesday, June 21, 2017

    Di Maria jela mwaka mmoja


    Madrid,Hispania.

    WINGA wa kimataifa wa Argentina,Angel Di Maria amehukumiwa kwenda jela kwa kipindi cha mwaka mmoja pamoja na kutozwa faini ya £1.76m baada ya kukiri kukwepa kodi wakati akiichezea Real Madrid.

    Di Maria ambaye kwa sasa anaichezea Paris Saint-Germain ya Ufaransa amekiri kufanya makosa mawili ya kukwepa kodi ambapo kila kosa moja adhabu yake ni kifungo cha miezi sita jela.

    Serikali ya Hispania imemtia hatiani Di Maria baada ya kubaini kuwa alikwepa kodi inayofikia £1.14m kati ya mwaka 2010 na 2014 wakati akiichezea Real Madrid.

    Hata hivyo Di Maria mwenye umri wa miaka 29 hatakwenda jela kama ilivyoamuliwa kwani sheria za Hispania hutoa msamaha kwa watu ambao wanakuwa wamefanya kosa kwa mara ya kwanza. 

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Di Maria jela mwaka mmoja Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top