728x90 AdSpace

  • Latest News

    Friday, June 30, 2017

    WADAU WA SOKA LA ZANZIBAR WAMWAGIA VIFAA BEKI MPYA WA YANGA





    Zanzibar.

    MLINZI mpya wa Yanga SC , Abdallah Haji Shaibu 'Ninja' amekabidhiwa vifaa vya michezo na wadau wake waliopo kisiwani Zanzibar.
    “Nawashakuru sana mashabiki wangu ambao wamekuwa nami toka naanza kucheza soka , Binafsi napenda kuvaa jezi namba 13, hiyo jezi nimekuwa nikiipenda tangu zamani kwa sababu kuna shabiki wangu mmoja wakati najiunga na Taifa Jang'ombe aliwahi kuniambia huwa anapenda anione nikiitumia, kwa kuwa namkubali nikaona niitumie na nimekuwa nikiipenda sana.
    “Nimekuja Yanga wamenipa jezi namba sita kutokana na ile niliyokuwa naipenda kuwa na mtu, sikuwa na jinsi kwa sababu naamini hata hii haiwezi kuniharibia kitu kwenye malengo yangu ndani ya Yanga ingawa ningepata ninayotaka ingekuwa vizuri,” alisema Ninja.
    Wiki iliyopita Mashabiki walifika kumpokea Ninja alipowasili akitokea Tanzania bara , Mashabiki hao walianza kumpokea tangu Bandarini Malindi na kumpandisha gari aina ya Canter hadi nyumbani kwao Jang’ombe huku njiani wakimuimbia nyimbo na kupiga dufu kuashiria furaha ya mpendwa wao huyo kusajiliwa Yanga.
    Siku ya Ijumaa ya June 23 Saa 3:00 za usiku katika Uwanja wa Amaan mchezaji huyo aliwaaga Mashabiki wake katika mchezo maalum kati ya Taifa ya Jang’ombe dhidi Mlandege SC. Ninja anatajwa kama mrithi wa Nadir Haroub Cannavaro.

    TANGAZA BIASHARA YAKO NASI Simu : + 255 675 734 252 + 255 717 705 548 Email : sokaextra82@gmail.com
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: WADAU WA SOKA LA ZANZIBAR WAMWAGIA VIFAA BEKI MPYA WA YANGA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top