728x90 AdSpace

  • Latest News

    Friday, June 30, 2017

    ASILIMIA 85 MSUVA ANASEPA YANGA SC.


    Dar Es Salaam.Uongozi wa klabu ya Yanga umethibitisha kufanya mazungumzo na klabu ya Difaa El Jadida inayoshiriki ligi kuu nchini Morocco ikitaka kumsajili winga Simon Msuva. Timu hiyo ambayo awali ilitaka kutumia njia za panya kumnasa Msuva, imekubali kukaa mezani na uongozi wa Yanga na sasa mazungumzo baina ya pande mbili yamefikia pazuri.

    Akizungumza kupitia Kipindi cha Spoti Hausi kinachorushwa na Globaltv Online, Kaimu Mkuu wa Kitendo cha Habari cha Yanga, Godlisten Anderson ‘Chicharito’, amesema kuwa wao kama uongozi wa Yanga wanaendelea ambapo kuna asilimia 85 za Msuva kuondoka ndani ya kikosi cha Yanga.

    “Ndani ya muda mfupi kila kitu kuhusiana na suala la Msuva kwenda Morocco kitakuwa wazi ambapo kwa sasa viongozi wanaendelea kulishughulikia kuhakikisha Msuva anaenda kukipiga nchini humo.

    “Kuna asilimia 85 ya yeye kuondoka na tayari tumeshawaandaa baadhi ya wachezaji kuziba pengo lake pale atakapoondoka ambapo kuna wachezaji kama Juma Mahadhi wanaweza kuziba nafasi yake pale atapoondoka,” alisema Chicharito.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: ASILIMIA 85 MSUVA ANASEPA YANGA SC. Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top