728x90 AdSpace

  • Latest News

    Saturday, June 24, 2017

    GEORGE LWANDAMINA MBIONI KUIKACHA YANGA


    Nairobi,Kenya.

    KOCHA wa mabingwa wa soka Tanzania,Yanga SC Mzambia George Lwandamina 'Chicken' huenda akaikacha timu hivi karibuni baada ya kutajwa kwenye orodha ya makocha 12 walioonyesha nia ya kuwania kibarua cha kuwanoa mabingwa wa kombe la SportPesa,Gor Mahia ya Kenya.

    Lwandamina aliyejiunga na Yanga SC mwishoni mwa mwaka jana akitokea Zesco United ameripotiwa na mtandao wa Kenya wa soka25east.com kuwa anawania nafasi iliyoachwa wazi na Mbrazil Ze Maria aliyetimkia FK Tirana inayoshiriki ligi daraja la pili nchini Albania. 

    Wengine walioonyesha nia ya kutaka kuifundisha Gor Mahia ni Mserbia Dravko Logarusic aliyewahi kuinoa timu hiyo siku za nyuma pamoja na Luc Eymal ambaye ni kocha wa zamani wa AFC Leopards.

    Kwa sasa Gor Mahia inanolewa na kocha wake msaidizi,Zedekiah Otieno ambaye pia yumo kwenye orodha ya makocha wanaowania kumrithi Ze Maria.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: GEORGE LWANDAMINA MBIONI KUIKACHA YANGA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top