Kazan,Urusi.
CHILE na Ujerumani zimeshindwa kutambiana baada ya usiku huu kutoka sare ya kufungana bao 1-1 katika mchezo wa mkali wa kundi B wa kombe la mabara uliochezwa kwenye uwanja wa Kazan Arena huko Kazan, Urusi.
Alexis Sanchez aliipa Chile uongoza katika dakika ya 6 baada ya kuifungia bao akimalizia pasi safi kutoka kwa kiungo, Arturo Vidal.
Bao hilo ambalo ni la 38 limemfanya Sanchez kuwa mfungaji bora wa muda wote wa Chile mbele ya gwiji Marcelo Salas mwenye mabao 37.
Lars Stindl aliisawazishia bao Ujerumani katika dakika ya 41 ya mchezo baada ya kugongeana vyema na wachezaji wenzake na kufanya mchezo uishe kwa sare ya bao 1-1.Hilo limekuwa ni bao la pili kufungwa na Stindl kwenye michuano ya mwaka huu.
Sasa hii ina maana kwamba hakuna timu yoyote ile kutoka kundi B iliyofanikiwa kutinga hatua inayofuatia ya nusu fainali.Chile na Ujerumani zinaongoza kundi baada ya kujikisanyia pointi 4 katika michezo yao miwili ya awali.
Cameroon na Australia zinashika nafasi ya tatu na ya nne baada ya kujikisanyia pointi 1 katika michezo yao miwili ya awali.Ikiwa zitashinda michezo yao ya Jumapili dhidi ya Chile na Ujerumani kwa tofauti ya bao tatu zitafuzu nusu fainali.
0 comments:
Post a Comment