St Petersburg,Urusi.
WENYEJI Urusi wameianza vyema michuano ya mwaka huu ya kombe la mabara baada ya jioni ya leo kuifunga New Zealand mabao 2-0 katika mchezo wa kundi A uliochezwa katika uwanja wa Stadion Krestovskyi.
Mabao yaliyoipa Urusi ushindi huo mzuri yamefungwa na Denis Glushakov katika dakika ya 31 na Fedor Smolov katika dakika ya 69.
Mchezo mwingine wa kundi A utachezwa kesho ambapo mawingwa wa Ulaya,Ureno watavaana na mabingwa wa Amerika Kaskazini Mexico.
Ikumbukwe michuano ya kombe la mabara huchezwa mwaka mmoja kabla ya kombe la dunia na hushirikisha timu nane kutoka mabara saba.Kila bara huwakilishwa na timu moja pamoja na mwenyeji.
0 comments:
Post a Comment