Lyon,Ufaransa.
MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Burkina Faso ,Bertrand Traore leo Jumatatu ameihama klabu ya Chelsea na kujiunga na klabu ya Olympique Lyon ya nchini Ufaransa kwa ada ya €20m.
Traore mwenye umri wa miaka 21 amejiunga na Olympique Lyon kwa makubaliano ya uhamisho ya mkataba wa miaka minne baada ya kufuzu vipimo vyake vya afya.
Olympique Lyon imeamua kumsajili Traore ikiwa ni sehemu ya maandalizi yake ya kujiandaa na maisha bila ya mshambuliaji wake mahiri,Alexander Lacazetti ambaye ameripotiwa kuwa na mpango wa kuhamia Arsenal.
Msimu uliopita Traore aliichezea klabu ya Ajax ya Uholanzi kwa mkopo wa msimu mmoja.Akiwa na Ajax,Traore aliiwezesha klabu hiyo ya Amsterdam Arena kushika nafasi ya pili kwenye ligi kuu ya Uholanzi pamoja na kufika fainali ya kombe la Europa Ligi.
Traore alijiunga na Chelsea mwaka 2013 na msimu mmoja alipandishwa kikosi cha kwanza na kufanikiwa kuanza kwenye michezo minne peke yake.
0 comments:
Post a Comment