728x90 AdSpace

  • Latest News

    Wednesday, June 28, 2017

    TETESI ZA USAJILI KUTOKA BARANI ULAYA JUMATANO YA LEO

    Alexander Lacazette

    Rais wa Lyon,Jean-Michel Aulas anaamini mshambuliaji wake Mfaransa,Alexandre Lacazette hataihama timu hiyo katika kipindi hiki cha usajili barani Ulaya licha ya kuwepo kwa tetesi kuwa anawindwa na Arsenal.Akifanya mahojiano na kituo cha habari cha Canal Plus, Aulas ameongeza kuwa upo uwezekano mkubwa kuwa mshambuliaji huyo akajiunga na Atletico Madrid mwezi Januari mwakani pindi adhabu yao ya kutosajili itakapokuwa imekwisha.(The Sun)

    Tottenham imeingia kwenye orodha ndefu ya vilabu vinavyoisaka saini ya beki wa kulia wa Southampton Cedric Soares mwenye umri wa miaka 25.Tottenham inamtazama Soares kama mbadala sahihi wa beki wake wa kulia Kyle Walker anayehusishwa na mpango wa kutimkia Manchester City.(Daily Mail)

    Mchakato wa Manchester United kumsajili mshambuliaji wa Real Madrid Alvaro Morata,24, unasuasua baada ya Real kupandisha dau la mchezaji huyo hadi karibu pauni milioni 80 (Mirror).

    Tottenham wapo tayari kumpa mkataba mpya beki wake Toby Alderweireld, 28, ambaye ananyatiwa na Inter Milan (Daily Mirror).

    Mshambuliaji wa Sunderland Jermain Defoe,34, amekwama kwa sababu Bournemouth na
    West Ham zinachelea kumchukua kutokana na
    gharama kubwa za mchezaji huyo (Daily
    Star).

    Mshambuliaji wa Burnley Andre Gray, 26,anataka mkataba mpya wenye mshahara wa pauni 100,000 kwa wiki, lakini klabu hiyo
    inasema haina uwezo wa kumlipa (Daily Star).

    Fernabahce ya Uturuki inafikiria kupanda dau la kumchukua winga wa Everton Kevin Mirallas, 29 (Fanatik).

    AC Milan wamejitoa katika mbio za kutaka kumsajili kiungo wa Real Madrid, James Rodriguez, 25, na hivyo kuwapa matumaini
    zaidi Chelsea na Manchester United (Mundo Deportivo).

    Everton wamewazidi kete Manchester United
    katika kumsajili beki Michael Keane, 24,kutoka Burnley na anatarajiwa kutua Goodison Park siku chache zijazo (Sun).

    Kurt Zouma au Michy Batshuayi, mmoja wao huenda akauzwa Sevilla,kama sehemu ya mkataba wa Chelsea kumsajili winga Vitolo (Express).

    Manchester United wanataka kumsajili kiungo wa Middlesbrough Marten de Roon, 26, na wanaamini anaweza kupatikana kwa pauni milioni 8.8 (Tutto Mercato).

    Chelsea, Tottenham, Everton, Leicester,Southampton na Stoke, zote zinamtaka Ben
    Gibson, 24, lakini watalazimika kulipa pauni milioni 25 kumpata beki huyo wa Middlesbrough (Daily Star).

    Tottenham wanamtaka beki wa Southampton Cedric Soares, 25, lakini wanakabiliwa na upinzani kutoka Barcelona na Juventus (Daily Mirror).

    Kiungo wa Leicester Nampalys Mendy, 25,anataka kwenda Bordeaux baada ya kushindwa kucheza vizuri England (L’Equipe).

    Barcelona wamekasirishwa na nahodha wao wa zamani Carlos Puyol, baada ya mmoja wa mabeki anaowawakilisha mwenye umri wa miaka 16, Eric Garcia kuamua kuitosa Barcelona na kwenda Manchester City (Independent).

    Paris Saint-Germain wanajiandaa kutoa euro milioni 240 kujaribu kuwashawishi Kylian Mbappe na kipa Gianluigi Donnarumma. PSG watatoa euro milioni 135 kwa ajli ya Mbappe na euro milioni 39 kwa ajili ya kipa wa AC Milan Donnarumma, na pia wanataka kutoa euro milioni 42 kumtaka Fabinho wa Monaco na euro milioni 23 kumchukua Raphael Guerrerro kutoka Borussia Dortmund (Sport).

    Tianjin Quanjian ya China iko tayari kurejea tena katika mbio za kutaka kumsajili mshambuliaji wa Borussia Dortmund Pierre Emerick-Aubameyang na wapo tayari kutoa euro milioni 80 (SportBild).

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: TETESI ZA USAJILI KUTOKA BARANI ULAYA JUMATANO YA LEO Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top