728x90 AdSpace

  • Latest News

    Sunday, June 25, 2017

    TAIFA STARS YAANZA VYEMA COSAFA ,YAITUNGUA MALAWI 2-0


    Rustenburg, Afrika Kusini.

    TIMU ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars imeanza vyema kusaka tiketi ya kutinga robo fainali ya michuano ya COSAFA CASTLE baada ya jioni ya leo kuifunga timu ya taifa ya Malawi,The Flames mabao 2-0 kwenye mchezo wa kwanza wa kundi A uliochezwa kwenye uwanja wa Moruleng huko Rustenburg, Afrika Kusini.

    Iliwachukua Taifa Stars dakika 13 kuandika bao la kwanza kupitia kwa winga wake wa kushoto,Shiza Ramadhani Kichuya.Kichuya alifunga bao hilo akiunganisha krosi safi kutoka kwa Simon Msuva.

    Dakika ya 18 Shiza Kichuya aliiandikia Taifa Stars bao la pili kwa shuti la mbali lililomshinda kipa wa Malawi na kutinga wavuni.Taifa Stars itarejea tena dimbani katikati ya wiki ijayo kucheza mchezo wake wa pili kwa kuvaana na Ushelisheli.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: TAIFA STARS YAANZA VYEMA COSAFA ,YAITUNGUA MALAWI 2-0 Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top