728x90 AdSpace

  • Latest News

    Friday, June 23, 2017

    PELLEGRINO KOCHA MPYA SOUTHAMPTON


    Southampton, England.

    KLABU ya Southampton inayoshiriki ligi kuu ya soka nchini England leo imemtangaza Muargentina, Mauricio Pellegrino kuwa kocha wake mkuu mpya.

    Pellegrino mwenye umri wa miaka 45 amekubali mkataba wa miaka mitatu kuchukua nafasi ya Mfaransa,Claude Puel aliyetimuliwa mapema mwezi huu baada ya kuhudumu kwa msimu mmoja.

    Kabla ya kutua Southampton,Pellegrino alikuwa akiifundisha Alaves ya Hispania iliyomaliza katika nafasi ya nane kwenye msimamo wa ligi ya La Liga.

    Mei mwaka huu Pellegrino alitangaza kujiuzulu kuifundisha Alaves baada ya klabu hiyo kufungwa na Barcelona kwenye mchezo wa fainali ya kombe la Copa Del Rey.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: PELLEGRINO KOCHA MPYA SOUTHAMPTON Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top