728x90 AdSpace

  • Latest News

    Sunday, June 25, 2017

    NELSON MANDELA KUKIPIGA BUNDESLIGA MSIMU UJAO


    Frankfurt,Ujerumani.

    KLABU ya Eintracht Frankfurt ya nchini Ujerumani imempa mkataba wa kulipwa mshambuliaji wake kinda kutoka Cameroon,Nelson Mandela.

    Mandela,18, ambaye jina lake kamili ni Nelson Mandela Mbouhom alipewa jina hilo na wazazi wake ambao walikuwa na mapenzi makubwa na Rais wa zamani wa Afrika Kusini,Nelson Mandela aliyefariki dunia mwaka 2013.

    Mandela alianzia soka lake kwenye shule ya watoto ya Barcelona ya La Masia kabla ya kuhama akiwa na miaka 13 na kuhamia Ujerumani akikokwenda kujiunga na Hoffenheim. 


    Mandela alidumu Hoffenheim kwa msimu mmoja pekee kabla ya kunyakuliwa na Eintracht Frankfurt ambayo baada ya kunogewa na vitu vyake imeamua kumpa mkataba mnono na kumpandisha kwenye kikosi chake cha kwanza tayari kwa msimu ujao wa ligi ya Bundesliga.

    Msimu uliopita Mandela aliwashitua vigogo wa klabu yake ya Eintracht Frankfurt baada ya kukifungia kikosi chake cha wachezaji wenye umri wa chini ya miaka 19 mabao manane katika michezo 14.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: NELSON MANDELA KUKIPIGA BUNDESLIGA MSIMU UJAO Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top