Liverpool,England.
LIVERPOOL haimuhitaji kikosini mlinzi wake wa kushoto,Alberto Moreno lakini pia haiko tayari kuona raia huyo wa Hispania anaondoka Merseyside kwa dau dogo hii ni baada ya leo Alhamisi kuikataa ofa ya £11m kutoka Napoli ya Italia.
Kwa mujibu wa mtandao wa Liverpool Echo habari zinasema kuwa Liverpool inataka kumuuza Moreno kwa dau la £15m.Dau ambalo ni sawa na lile ililolitoa mwaka 2015 wakati inamnunua mlinzi huyo kutoka Sevilla.
Habari zaidi zinasema Liverpool haitaki kufanya haraka kumuuza Moreno kwani tayari kuna vilabu ambavyo vimeshaonyesha nia ya kumtaka hivyo inaamini itapata klabu itakayotoa dau zuri.
Liverpool imeamua kumweka sokoni Moreno baada ya mlinzi huyo kushindwa kujihakikishia namba ya kudumu kwenye kikosi cha kwanza cha kocha Jurgen Klopp.
Msimu uliopita Moreno alifanikiwa kuanza kikosi cha katika michezo miwili pekee huku sehemu kubwa ya michezo ikichezwa na James Milner ambaye ni mchezaji wa safu ya kiungo.
0 comments:
Post a Comment