728x90 AdSpace

  • Latest News

    Tuesday, June 20, 2017

    Majimaji FC yapiga chini nyota wake 16


    Songea,Tanzania.

    UONGOZI wa Klabu ya  Majimaji FC umeachana na wachezaji wake 16 walioitumikia msimu uliopita wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

    Wachezaji waliotemwa ni kipa Agathon Antony, Kutche Bidual, Peter Joseph,Emanuel Semwanza, Paul Nyange, Taria Simba, Said Mrisho na Seleman Kibuta.

    Wengine ni Mfanyeje Mussa, George Mpole,Yusuph Mgwao, Adam Siba, Wazir Salum,Bahati Yusuph,Ibrahim Mohamed na Sadat Mohamed.

    Katibu Mkuu wa Majimaji,Zakharia Mgalimayo, amesema wachezaji hao wengi ni wale waliomaliza mikataba yao na kwa mujibu wa ripoti ya kocha wa timu hiyo, Kali Ongala,walishindwa kukidhi matarajio.

    “Kila tunachokifanya ni kwa mujibu wa ripoti ya kocha, hivyo kuachana na wachezaji hao kunatoa nafasi ya kuwasajili wengine bora zaidi, kwani mipango yetu ni kuhakikisha tunakuwa na kikosi imara cha ushindani msimu ujao, ukizingatia msimu uliopita tuliponea chupuchupu kushuka daraja,” alisema.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Majimaji FC yapiga chini nyota wake 16 Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top