728x90 AdSpace

  • Latest News

    Saturday, June 24, 2017

    MTANZANIA FARID MUSSA NA TENERIFE YAKE WANA DAKIKA 90 TU LEO ZA KUTINGA LA LIGA


    Getafe,Hispania.

    WINGA mahiri wa zamani wa Azam FC,Farid Mussa huenda Jumamosi ya leo akaandika historia ya kuwa Mtanzania wa kwanza kucheza ligi ya juu nchini Hispania maarufu kama La Liga pale timu yake ya CD Tenerife itakaposhuka kwenye uwanja wa ugenini wa Coliseum Alfonso PĂ©rez mishale ya saa 4:00 Usiku kucheza na Getafe kwenye mchezo wa marudiano wa kuwania tiketi moja iliyosalia ya kupanda daraja.

    Katika mchezo wa awali uliochezwa kwenye uwanja wa Heliodoro Rodriguez Lopez wenyeji CD Tenerife walishinda kwa bao 1-0 lililofungwa na Jorge Saenz kwa kichwa katika dakika ya 21 akiunganisha krosi ya Mjapani Gaku Shibasaki.

    CD Tenerife inaingia kwenye mchezo wa leo ikihitaji kupata sare ama ushindi wa aina yoyote ile ili iweze kupanda daraja kwa mara ya tangu mwaka 2009.

    Farid Mussa alijiunga na CD Tenerife akitokea Azam FC mwishoni mwa mwaka jana baada ya kufuzu majaribio yake ya wiki mbili.



    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: MTANZANIA FARID MUSSA NA TENERIFE YAKE WANA DAKIKA 90 TU LEO ZA KUTINGA LA LIGA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top