Kampala,Uganda.
MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Uganda, Emmanuel Okwi amekanusha kufikia makubaliano ya kurejea Simba SC.
Okwi ambaye msimu uliopita aliichezea SC Villa (Jogoo) ya nyumbani kwao Uganda ametumia ukurasa wake wa twitter kukanusha habari zilizoenea kuwa amekubali kurejea Simba SC kwa mkataba wa miaka miwili.
Juzi Alhamisi vyombo vingi vya habari nchini viliripoti kuwa katikati ya wiki hii Okwi alikutana na kiongozi mmoja wa juu wa Simba SC kwenye hoteli moja huko Uganda na kufikia makubaliano ya kurejea Simba SC kuchukua nafasi ya Ibrahim Ajibu anayedaiwa kuwa mbioni kujiunga na Yanga SC.
Ikumbukwe Okwi aliwahi kuichezea Simba SC kwa misimu kadhaa nyuma kabla ya kuihama miaka miwili iliyopita na kutimkia nchini Denmark kujiunga na timu ya Sonderjyske.
Akiwa Sonderjyske Okwi alishindwa kuwika na kuamua kurejea nyumbani kwao Uganda na kujiunga AS Villa kwa mkataba wa miezi sita ambao tayari umekwisha.
0 comments:
Post a Comment