Paul Manjale,Dar Es Salaam.
MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Zimbabwe,Donald Ndombo Ngoma hatimaye amemaliza utata wa timu ipi ataichezea katika msimu ujao wa soka hii ni baada ya mchana wa leo kusaini kandarasi mpya ya miaka miwili ya kuendelea kuwatumikia mabingwa watetezi wa ligi kuu bara,Yanga SC.
Ngoma ,27, ambaye alikuwa akihusishwa na mpango wa kutaka kutimkia Simba SC pamoja na Polokwane City ya Afrika Kusini ameridhia kusaini kandarasi hiyo mpya baada ya kufikia makubaliano binafsi na Yanga SC ambayo imeonyesha nia ya kuendelea kuhitaji huduma yake.
0 comments:
Post a Comment