Kigali,Rwanda.
MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Burundi,Laudit Mavugo ameripotiwa na mtandao wa Kenya wa Soka25east.com kuwa amekubali dili la kujiunga na klabu yake ya zamani ya AS Kigali inayoshiriki ligi kuu ya soka nchini Rwanda.
Mtandao huo umedai kuwa Mavugo mwenye umri wa miaka 23 amekubali mkataba wa miaka miwili wa kujiunga na AS Kigali akitokea Simba SC ya Dar Es Salaam kwa dau ambalo halijawekwa wazi thamani yake.
Mavugo alijiunga na Simba SC mwezi Agosti mwaka jana akitokea Vital’O ya nyumbani kwao Burundi kwa mkataba wa miaka miwili kwa dau la zaidi ya Shilingi Milioni 100 za Tanzania.
Kama habari hizi zitakuwa kweli,Mavugo atakuwa ametumikia mwaka mmoja kati ya miwili iliyo kwenye mkataba wake uliotarajiwa kufika mwisho Agosti mwakani.BOFYA HAPA KWA HABARI ZAIDI
0 comments:
Post a Comment