728x90 AdSpace

  • Latest News

    Monday, June 26, 2017

    JOSE MOURINHO AFIWA NA BABA YAKE MZAZI


    Setubal,Ureno.

    KOCHA wa Manchester United mwenye mbwembwe na maneno mengi Mreno, Jose Mourinho amefiwa na baba yake mzazi, Félix Mourinho.

    Félix amefariki amefariki usiku wa kuamkia leo huko Setubal,Ureno akiwa na umri wa miaka 79 kwa ugonjwa wa kiharusi.

    Wakati wa uhai wake Félix alicheza soka kwa kipindi cha miaka 20 akividakia vilabu vya Vitoria de Setubal na Belenenses kabla ya kutundika daruga na kuamua kuwa kocha.

    Vilabu ambavyo Félix aliwahi kuvifundisha ni pamoja na Estrela de Portalegre,Caldas, União de Leiria, Amora, Rio Ave,Belenenses, Varzim,União da Madeira, O Elvas, Paredes, Benfica,Castelo Branco,União de Santarém and Vitória de Setúbal.

    Félix anatarajiwa kuzikwa siku ya Alhamisi huko nyumbani kwake Setubal.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: JOSE MOURINHO AFIWA NA BABA YAKE MZAZI Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top