Sochi,Urusi.
UJERUMANI imeungana na Chile kufuzu fainali ya michuano ya mwaka huu ya kombe la mabara baada ya Alhamisi kuifunga Mexico mabao 4-1 kwenye mchezo wa nusu fainali uliochezwa huko Olimpiyskiy Stadion,Sochi,Urusi.
Mabao ya Ujerumani yamefungwa na Leon Goretzka aliyefunga mabao mawili dakika ya 6 na 8,Timo Werner dakika ya 59 na Amin Younes dakika ya 91 .Bao la Mexico limefungwa dakika ya 89 na Marco Fabian kwa mkwaju wa mita 35.
Sasa Ujerumani na Chile zitavaana siku ya Jumapili kwenye mchezo wa fainali utakaochwa huko St Petersburg huku Mexico na Ureno zikicheza mapema kusana mshindi wa tatu.
0 comments:
Post a Comment