Abidjan,Ivory Coast.
ASEC Mimosas ndiyo mabingwa wapya wa ligi kuu ya nchini Ivory Coast kwa msimu wa 2016/17 baada ya jana Jumamosi jioni kuishindilia Williamsville Athletic Club bao 1-0 huko Bouake na kutwaa ubingwa wake 25.
Shukrani za dhati ziende kwa mshambuliaji wa kimataifa wa Burkina Faso,Aristide Bance,33, aliyefunga bao hilo pekee kwa mkwaju wa penati katika dakika ya 77 na kuipa ASEC Mimosas ubingwa wake wa kwanza baada ya kuusotea kwa miaka saba.
Bance ameanza kujipatia jina nchini Tanzania baada ya hivi karibuni vyombo mbalimbali vya habari hasa magazeti kuripotiwa kuwa mshambuliaji huyo mwenye umbo mrefu anawindwa na mabingwa wa ligi kuu bara,Yanga SC.
Kabla ya kutua ASEC Mimosas,Bance amewahi kucheza soka la ushindani kwenye vilabu visivyopungua 19 vya Ulaya na Afrika.Baadhi ya vilabu hivyo ni pamoja na FC Augsburg na Mainz 05 vya Ujerumani,Roga FC ya Latvia na Chippa United ya Afrika Kusini.
0 comments:
Post a Comment