Dar Es Salaam,Tanzania.
KATIKA kuhakikisha kuwa inakuwa na kikosi kipana na kitakachotisha kwenye msimu ujao wa ligi kuu bara,Singida United leo imemsajili beki wa kati wa Mshikamano FC inayoshiriki ligi daraja la kwanza Taifa,Rolland Msonjo
Msonjo mwenye umri wa miaka 19 amejiunga na Singida United kwa mkataba wa miaka miwili kwa dau ambalo halijawekwa wazi.
Singida United imemsajili Msonjo baada ya kuvutiwa na uwezo wake tangu alipotua kikosi hapo kwa mara ya kwanza mwanzoni mwa mwezi huu.
Msonjo alikuwa sehemu ya kikosi cha Singida United ambacho kirishiriki michuno ya SportPesa na kuondolewa kwa matuta na AFC Leopards ya Kenya.
0 comments:
Post a Comment