728x90 AdSpace

  • Latest News

    Sunday, June 25, 2017

    MGANDA EMMANUEL OKWI AANGUKA MIAKA MIWILI MSIMBAZI


    Paul Manjale,Dar Es Salaam.

    HATIMAYE kiungo mshambuliaji wa kimataifa wa Uganda,Emmanuel Okwi amekata mzizi wa fitina baada ya kuingia kandarasi ya miaka miwili ya kujiunga na Wekundu wa Msimbazi,Simba SC.

    OKwi ambaye aliwasili nchini jana usiku akitokea nyumbani kwako Uganda alikokuwa akiichezea Sports Club Villa ameingia kandarasi hiyo usiku huu chini ya uratibu wa Makamu wa Rais wa Simba SC,Geoffrey Nyange Kaburu.

    Okwi anakuwa mchezaji wa kwanza wa kigeni kujiunga na Simba SC tangu dirisha la usajili wa wachezaji lilipofunguliwa Juni 15 mwaka huu.

    Mpaka sasa Simba SC ambayo msimu ujao itashiriki michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika imefanikiwa kuwanasa wachezaji saba wapya.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: MGANDA EMMANUEL OKWI AANGUKA MIAKA MIWILI MSIMBAZI Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top