Dar Es Salaam,Tanzania.
KIUNGO mahiri wa Rwanda, Haruna Hakizimana Niyonzima amezima uvumi ulioenea kuwa alikuwa kwenye mazungumzo ya kujiunga na mabingwa wa kombe la FA,Simba SC baada ya jioni ya leo kusaini mkataba mpya wa miaka miwili wa kuendelea kuwachezea mabingwa wa soka Tanzania,Yanga SC.
Niyonzima amesaini mkataba huo baada ya ule wa awali wa miaka miwili kuwa umekwisha na kuibua hisia kuwa kiungo huyo wa zamani wa APR angetimka Jangwani.
Kusaini mkataba mpya kwa Niyonzima ni pigo kubwa kwa mashabiki wa Simba SC ambao walidhani wangemnasa kiungo huyo mwenye mbwembwe na ufundi mwingi awapo uwanjani.
Niyonzima alijiunga na Yanga SC miaka sita iliyopita akitokea APR ya nyumbani kwao Rwanda.
0 comments:
Post a Comment