728x90 AdSpace

  • Latest News

    Wednesday, June 21, 2017

    MABARA:Ronaldo aitungua Urusi


    Moscow,Urusi.

    BAO la kichwa la nahodha Cristiano Ronaldo limeipa Ureno ushindi wa bao 1-0 dhidi ya wenyeji Urusi katika mchezo wa pili wa kundi A wa kombe la mabara ulioisha hivi punde kwenye uwanja wa Spartak huko Moscow.

    Ronaldo alifunga bao hilo kwa kichwa katika dakika ya 8 akiunganisha krosi ya mlinzi Raphael Guerrero kutoka wingi ya kushoto na kupiga kichwa kilichokwenda juu kidogo ya kipa wa Urusi,Igor Akinfeev aliyekuwa akicheza mchezo wake wa 100.

    Bao hilo ambalo ni la 74 kwa Ronaldo,32,katika michezo 141 aliyoichezea Ureno limeipeleka timu hiyo kileleni mwa msimamo wa kundi A baada ya kufikosha pointi nne.Pointi moja mbele ya Urusi yenye pointi tatu. 

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: MABARA:Ronaldo aitungua Urusi Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top