Monaco,Ufaransa.
MABINGWA wa Ufaransa AS Monaco wametangaza kumsajili kiungo mkabaji wa Lille,Soualiho Meite kwa ada ya uhamisho ya Euro Milioni 8.
Meite mwenye umri wa miaka 23 amejiunga na AS Monaco kwa mkataba wa miaka mitano baada ya kufaulu vipimo vyake ya afya.
AS Monaco imemsajili Meite baada ya kuvutiwa na kiwango alichokionyesha msimu uliopita wakati alipokuwa anaichezea Zulte Waregem ya Ubelgiji kwa mkopo.
Akiwa na Zulte Waregem Meite aliiwezesha timu hiyo kutwaa ubingwa wa kombe la Ubelgiji.Akicheza michezo 30 na kufunga bao moja huku akipika bao moja.
Méité anakuwa mchezaji wa nne kujiunga na AS Monaco tangu kufungulia kwa dirisha la usajili mapema mwezi huu.Wengine ni Diego Benaglio,Jordy Gaspar na Youri Tielemans.
0 comments:
Post a Comment