Madrid,Hispania.
JAMAA kashindikana.Hii ndiyo kauli pekee unayoweza kuitumia kumwelezea Rais wa sasa wa klabu ya Real Madrid ya Hispania,Florentino Pérez.
Ishu iko hivi jamaa ameukwaa tena Urais wa klabu hiyo tajiri zaidi duniani baada ya kukosa mpinzani kwenye nafasi hiyo kubwa kabisa kwenye ngazi ya uongozi wa vilabu vya soka duniani.
Jana Jumapili ndiyo ilikuwa siku ya mwisho kwa wagombea wa nafasi ya Urais kutangaza nia lakini mpaka muda wa mwisho unafika hakuna mgombea hata mmoja aliyejitokeza kumpinga Pérez aliyeingia madarakani kwa mara ya mwaka 2000.
Taarifa iliyochapishwa leo asubuhi kwenye tovuti rasmi ya Real Madrid imesema Perez mwenye miaka 70 ataiongoza klabu hiyo kwa miaka mingine minne baada ya kuwa mgombea pekee kwenye uchaguzi uliotarajiwa kufanyika hivi karibuni.
Hii ni mara ya pili Perez anaukwaa Urais wa Real Madrid bila kupingwa.Awali ilikuwa ni mwaka 2013 pale alipoingia madarakani kirahisi bila ya kupata mtu wa kumpinga.
Perez aliingia madarakani kwa mara ya kwanza mwaka 2000 baada ya kumshinda Lorenzo Sanz kwa ahadi ya kumsajili nyota wa zamani wa Ureno,Luis Figo kutoka kwa wapinzani wao Barcelona.Jambo ambalo lilifanikiwa na Figo akajiunga na Real Madrid kwa dau la rekodi ya dunia la Euro Milioni 62.
Ugumu wa vigezo vya ugombea ndivyo zimedaiwa kuwakwamisha watu wengi kushindwa kugombea nafasi ya Urais klabuni Real Madrid kwani mtu ili awe na sifa ya kugombea wadhifa huo anapaswa kuwa ni mwanachama wa klabu hiyo kwa kipindi kisichopungua miaka 20.
Pia anapaswa kuwa kiasi cha fedha kisichopungua Euro Milioni 75 kwenye benki za Hispania.
0 comments:
Post a Comment