728x90 AdSpace

  • Latest News

    Thursday, June 22, 2017

    OSCAR AFUNGIWA MICHEZO MINANE NA KULIMWA FAINI YA SHILINGI MILIONI 13


    Beijing,China.

    KIUNGO wa zamani wa Chelsea,Oscar Dos Santos amefungiwa michezo minane pamoja na kutozwa faini na chama cha soka cha China (CFA) baada ya kusababisha ugomvi kati ya wachezaji wa timu yake ya Shanghai SIPG na wachezaji wa Guangzhou R&F.

    Jumapili iliyopita Oscar ,25, alisababisha ugomvi mkubwa baada ya kuwapiga kwa makusudi kwa mpira wachezaji wawili wa Guangzhou R&F na kuamsha hasira kali baina ya wachezaji wa timu zote mbili kwenye mchezo wa ugenini ulioisha kwa sare ya bao 1-1.

    Oscar pia ameamuliwa kulipa faini ya Yeni 40,000 za China ambazo ni sawa Shilingi Milioni 13 za Tanzania.

    Mbali ya Oscar wengine waliofungiwa ni pamoja na Fu Huan wa Shanghai SIPG aliyefungiwa michezo sita.Li Tixiang wa Guangzhou R&F yeye amefungiwa michezo mitano huku mwenzake Chen Zhizhao akifungiwa michezo saba.

    Wakati huohuo vilabu vya Shanghai SIPG na Guangzhou R&F navyo vimepigwa faini pamoja na kupewa kalipio kali kwa kushindwa kuwathibiti wachezaji wao.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: OSCAR AFUNGIWA MICHEZO MINANE NA KULIMWA FAINI YA SHILINGI MILIONI 13 Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top