728x90 AdSpace

  • Latest News

    Wednesday, June 28, 2017

    SELEMANI MATOLA KOCHA MPYA LIPULI FC


    Iringa,Tanzania.

    KOCHA Msaidizi wa zamani wa Simba,Selemani Matola, amesaini mkataba wa mwaka mmoja wa kuinoa Lipuli FC kitakachoshiriki Ligi Kuu Bara msimu ujao.

    Lipuli, yenye maskani yake mkoani Iringa, ni miongoni mwa timu tatu zilizofanikiwa kupanda Ligi Kuu, nyingine ni Singida United na Njombe Mji.

    Habari ambazo zimeufikia mtandao huu asubuhi ya leo ni zinasema Matola aliyewahi pia kuinoa Geita Gold Mine ya Geita atakianza kibarua chake hicho kipya kesho Alhamisi jijini Dar Es Salaam.

    Kikosi cha Lipuli FC kiko jijini Dar Es Salaam kwa ajili ya kambi ya kujiwinda na msimu mpya wa Ligi Kuu Bara inayotarajiwa kuanza mwezi Agosti mwaka huu.Lipuli FC itakuwa ikijifua kwenye Uwanja wa Karume.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: SELEMANI MATOLA KOCHA MPYA LIPULI FC Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top