728x90 AdSpace

  • Latest News

    Sunday, June 18, 2017

    EURO U-21:Asensio afunga hat-trick Hispania ikishinda 5-0 kundi B


    Gdynia,Poland.

    STAA wa Real Madrid,Marco Asensio amefunga mabao matatu (hat-trick) na kuiwezesha Hispania kuanza kwa mkwara mkubwa harakati zake za kuusaka Uchampion (Ubingwa) wa michuano ya soka ya Ulaya kwa wachezaji wenye umri wa chini ya miaka 21 baada ya Jumamosi usiku kuifunga Macedonia mabao 5-0 katika mchezo wa kundi B uliochezwa huko Stadion GOSiR Poland

    Saul Niguez wa Atletico Madrid ndiye aliyekuwa wa kwanza kuifungia bao Hispania baada ya kufunga kwa tiki taka katika dakika ya 10.Bao la pili lilifungwa na Asensio katika dakika ya 16 kabla ya Gerard Deulofeu kuifungia Hispania bao la tatu kwa mkwaju wa penati katika dakika ya 35.

    Mkwaju huo wa penati ulipatikana baada ya Egzon Bejtulai wa Macedonia kuunawa mpira akiwa ndani ya boksi na mwamuzi kuamua kuizawadia Hispania mkwaju wa penati.


    Katika dakika za 54 na 72,Asensio alitunisha ushindi wa Hispania baada ya kufunga mabao mawili na kukamilisha hat-trick yake iliyomfanya kuwa mchezaji wa pili kufunga mabao matatu akiwa na Ra Lojita baada ya Thiago Alcantara aliyefunga idadi hiyo ya mabao mwaka 2013.

    Katika mchezo mwingine wa kundi B,Ureno iliifunga Serbia mabao 2-0 yaliyofungwa na Goncalo Guedes pamoja na Bruno Fernandes.

    Michezo Ijayo Kundi B

    Jumanne: Hispania v Ureno
                      Serbia v Macedonia

    Ijumaa : Macedonia v Ureno
                   Serbia v Hispania
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: EURO U-21:Asensio afunga hat-trick Hispania ikishinda 5-0 kundi B Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top