Monaco,Ufaransa.
MONACO imesalimu amri mbele ya noti za matajiri wa Chelsea baada ya kukubali kumuuza kiungo wake mkabaji, Tiemoue Bakayoko kwa dau la £35.2m.
Makubaliano hayo yamefikiwa baada ya vilabu hivyo kuwa kwenye mazungumzo ya kipindi kirefu ya kutaka kuuziana kiungo huyo mwenye umri wa miaka 22.
Msimu uliopita Bakayoko alifanikiwa kuvitoa udenda vilabu vingi vikubwa baada ya kuonyesha kiwango cha juu cha usakataji kabumbu kilichoiwezesha Monaco kutwaa ubingwa wake wa kwanza wa Ligue 1 pamoja na kufika nusu fainali ya michuano ya klabu bingwa Ulaya.
Kusajiliwa kwa Bakayoko kumedaiwa huenda kukafungua milango kwa kiungo,Nemanja Matic anayehusishwa na mpango wa kutaka kuhamia Manchester United kwenda kuungana na kocha wake wa zamani José Mourinho.
0 comments:
Post a Comment