728x90 AdSpace

  • Latest News

    Tuesday, June 20, 2017

    SAFI:Wagombea 74 warejesha fomu TFF,zoezi lafungwa jioni ya leo


    Dar Es Salaam,Tanzania.

    WANAFAMILIA 74 wa mpira wa miguu,wamechukua na kurejesha fomu za kuwania nafasi mbalimbali za uongozi katika Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Agosti 12, mwaka huu.

    Hadi zoezi hilo linafungwa leo Juni 20, 2017 saa 10.00 jioni wagombea wote wamerejesha ambako kwenye nafasi ya Urais, jumla ya wagombea 10 walijitokeza kuomba nafasi hiyo wakati kwenye Makamu Rais
    wamejitokeza sita.

    Wadau 58 wamejitokeza kuwania nafasi za ujumbe wa kamati ya utendaji Katika Kanda mbalimbali. Zoezi la kuchukua na kurejesha fomu kwa mujibu wa Kanuni ya 10,limefanyika kwa siku tano kuanzia Juni 16,2017 hadi Juni 20, mwaka huu.

    Siku ya kwanza ilipoanza tu, Jamal Malinzi alikuwa wa kwanza kuchukua fomu na kurejesha huku akifuatiwa na Imani Madega,Wallace Karia, Fredrick Masolwa, Athumani Nyamlani, Fredrick Mwakalebela,John Kijumbe, Shija Richard, Ally Mayay na Emmanuel Kimbe.

    Waliojitokeza kuwania Makamu wa Rais na kurejesha fomu wako 

    Mulamu Ng’hambi,Michael Wambura, Geofrey Nyange, Mtemi Ramadhani, Robert Selasela na Stephen Mwakibolwa.

    Wajumbe wa Kamati ya Utendaji kwa kufuata Kanda 13 ni kama ifuatavyo:

    Kanda Na. 1 Mikoa ya Kagera na Geita;
    Soloum Chama
    Kaliro Samson
    Leopold Mukebezi
    Abdallah Mussa

    Kanda Na. 2 Mikoa ya Mara na Mwanza;

    Vedastus Lufano
    Ephraim Majinge
    Samwel Daniel
    Aaron Nyanda

    Kanda Na. 3 Mikoa ya Shinyanga na Simiyu;

    Benista Rugora
    Mbasha Matutu
    Stanslaus Nyongo

    Kanda Na. 4 Mikoa ya Arusha na Manyara;

    Omari Walii
    Sarah Chao
    Peter Temu

    Kanda Na. 5 Mikoa ya Kigoma na Tabora;

    John Kadutu
    Issa Bukuku
    Abubakar Zebo
    Francis Michael

    Kanda Na. 6 Mikoa ya Katavi na Rukwa;

    Kenneth Pesambili
    Baraka Mazengo

    Kanda Na. 7 Mikoa ya Mbeya, Songwe na Iringa;

    Elias Mwanjala
    Cyprian Kuyava
    Erick Ambakisye
    Abousuphyan Silliah

    Kanda Na. 8 Mikoa ya Njombe na Ruvuma;

    James Mhagama
    Golden Sanga
    Vicent Majili
    Yono Kevela

    Kanda Na. 9 Lindi na Mtwara;

    Athuman Kambi
    Dunstan Mkundi

    Kanda Na. 10 Mikoa ya Dodoma na Singida;

    Hussein Mwamba
    Mohamed Aden
    Mussa Sima
    Stewart Masima
    Ally Suru
    George Benedict

    Kanda Na. 11 Mikoa ya Pwani na Morogoro;

    Charles Mwakambaya Gabriel Makwawe
    Francis Ndulane
    Hassan Othman

    Kanda ya 12. Mikoa ya Kilimanjaro na Tanga

    Khalid Mohamed
    Goodluck Moshi
    Thabit Kandoro

    Kanda Na. 13 Mkoa wa Dar es Salaam

    Emmanuel Ashery
    Ayoub Nyenzi
    Saleh Alawi
    Shaffih Dauda
    Abdul Sauko
    Peter Mhinzi
    Ally Kamtande
    Said Tully
    Mussa Kisoky
    Lameck Nyambaya
    Ramadhani Nassib
    Aziz Khalfan
    Jamhuri Kihwelo
    Saad Kawemba
    Bakari Malima

    Kwa siku tatu, kuanzia kesho Juni 21 hadi 23,mwaka huu kwa mujibu wa kanuni ya 11.1 ya Uchaguzi wa TFF,Kamati ya Uchaguzi itaanza
    mchujo wa awali kwa wote waliojitokeza kuwania nafasi mbalimbali kama inavyojionesha hapo juu.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: SAFI:Wagombea 74 warejesha fomu TFF,zoezi lafungwa jioni ya leo Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top