London,England.
Bournemouth imefumba macho na kumsajili beki wa kati wa Chelsea,Nathan Ake kwa dau la rekodi la £20m.
Ake mwenye umri wa miaka 22 amejiunga na Bournemouth kwa mkataba wa miaka mitano na kuwa mchezaji ghali zaidi kuwahi kununuliwa na klabu hiyo.
Msimu uliopitaa,Ake anayetokea Uholanzi aliichezea Bournemouth kwa mkopo wa miezi sita na kuifungia mabao matatu kabla ya mwezi Januari kurejea Chelsea baada ya safu yake ya ulinzi kukumbwa na majeruhi.
Ake anakuwa mchezaji wa tatu kujiunga na Bournemouth katika kipindi hiki cha usajili barani Ulaya.Wengine ni Asmir Begovic aliyetokea Chelsea kwa dau £10m pamoja na Jermain Defoe aliyetokea Sunderland kwa uhamisho huru.
0 comments:
Post a Comment