728x90 AdSpace

  • Latest News

    Monday, June 19, 2017

    NOMA:Takuma Asano abaniwa kukipiga Arsenal


    London,England.

    MAJAALIWA ya mashabiki wa Arsenal kumuona nyota wao Mjapan,Takuma Asano akiichezea klabu hiyo kwenye msimu ujao wa ligi kuu na michuano mingine yamegonga mwamba baada ya mara nyingine kunyimwa  kibali cha kufanyia kazi nchini England.

    Taarifa zilizotoka leo mapema asubuhi zimesema Takuma mwenye miaka 22 hataichezea Arsenal msimu ujao na badala yake atasalia Stuttgart kwa msimu mmoja zaidi baada ya kushindwa kufikia baadhi ya vigezo vya kupata kibali cha kufanyia kazi nchini England.

    Sababu kuu inayodaiwa kumkosesha Takuma nafasi ya kuvaa jezi ya Arsenal msimu ujao ni kuwa na idadi ndogo ya michezo kwenye timu yake ya taifa ya Japan pamoja na kutokuwa na hati (pasi) ya kusafiria barani Ulaya.

    Takuma alijiunga na Arsenal Julai Mosi mwaka jana kwa ada ya £5m akitokea klabu ya Sanfrecce Hiroshima ya nyumbani kwao Japan.

    Takuma alishindwa kutimiza ndoto yake ya kucheza ligi kuu ya soka nchini England na kulazimika kujiunga na klabu ya Stuttgart ya Ujerumani kwa mkopo baada ya kukosa kibali cha  kazi.

    Akiwa na Stuttgart, Takuma aliisaidia klabu hiyo kongwe kupanda daraja na kurejea ligi ya Bundesliga baada ya kufunga mabao matano na kutengeneza mengine manne katika michezo 27.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: NOMA:Takuma Asano abaniwa kukipiga Arsenal Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top