London,England.
MABINGWA wa kihistoria wa kombe la FA nchini England,Arsenal wameripotiwa kuwa njiani kuelekea nchini Ubelgiji kuanza mchakato wa kumsajili kiungo wa ulinzi wa Genk,Sander Berge.
Taarifa kutoka gazeti la Daily Mirror la nchini England zinasema Arsenal imezimika kwa Berge mwenye miaka 19 baada ya kuvutiwa na ripoti walizopata kutoka kwa maskauti wao ambao kwa kipindi kirefu wamekuwa wakimfuatilia kiungo huyo anayeichezea pia timu ya taifa ya Norway.
Arsenal imeamua kumgeukia Berge baada ya viungo wake Francis Coquelin na Mohamed Elneny kushindwa kitimiza vyema majukumu yake yao ya kuilinda safu yao ya ulinzi pamoja na kuunganisha timu.
Mbali ya Arsenal vilabu vingine vinavyohusishwa na mpango wa kutaka kumsajili Berge mwenye thamani ya £18m ni pamoja na Sevilla, Monaco pamoja na Everton.
Berge alijiunga na Genk msimu uliopita akitokea Valerenga ya nyumbani kwao Norway ambayo mwaka 2016 ilikataa kumuuza kwenda Everton baada ya klabu hiyo ya jiji la Liverpool kumwandalia dau la £1.8m.
0 comments:
Post a Comment