728x90 AdSpace

  • Latest News

    Saturday, June 17, 2017

    KUBWA KULIKO:Ivo Mapunda Sports Centre imekuja na jambo jipya na jema kwako


    Dar Es Salaam,Tanzania.

    TUNAPENDA kuwapa taarifa wana michezo wote hapa nchini kwamba #ivomapunda_sports_center tutaandaa semina ya siku moja kwa makocha wa magolikipa na magolikipa
    wote na pia kwa makocha wa kawaida iwapo watapenda kuongeza ujuzi kwa faida yao.

    IVOMAPUNDA SPORTS CENTER kwa kushirikiana na KEEPERS FOUNDATION [ www.keepersfoundation.pl ]toka nchini POLAND watakuja kututembelea katika kituo chetu nakuona maendeleo yetu.

    MAREK DGAGOZS ni mmiliki wa kituo hicho na ni mkufunzi [instructor] wa kimataifa anaetambulika na FIFA.Hivyo kupitia kituo chetu tukamuomba atupe semina kidogo na amekubali.

    HIVYO tukaona ni vizuri hii semina tuwashirikishe wadau wote hasa MAGOLIKIPA NA WALIMU WAO ili kuongeza ufanisi mzuri kwenye idara ya GOALKEEPING ambayo ni nyeti sana.Hivyo nawaasa na nawaomba wadau wote kuhuzuria semina hiyo ambayo itakuwa kati ya tarehe 13 au 14 mwezi wa saba[mwezi ujao].

    Ratiba kamili tutaitoa punde baada ya mawasiliano na chama cha mpira nchini TFF ili watupe baraka zao na pia kutupa uwanja wa mazoezi kwa ajili ya tukio hilo muhimu.

    Kwa watakao hudhuria lazima uje ukiwa full kimazoezi kwani ni semina itakayokuwa na vitendo zaidi na muda wa kuanzia semina itakuwa ni saa 2:00 asubuhi.

    Wageni wetu watafika tarehe 12/07/2017 saa 8:40 mchana na watakuwa hapa nchini kwa siku tatu tu na kuendelea na safari nchini RWANDA.

    Kutakuwa na mchango wa shillingi 5000/- kwa ajili ya kununua maji kwa washiriki lakini pia tunaomba mchango wako mwananchi kutusapoti ili tufanikishe jambo hili.

    Taarifa zaidi ntakuwa naitoa kupitia mitandao ya kijamii na radio/tv. Kwa mawasiliano ili kushiriki au kupata full information utanipata kwa Namba 0677553308 na wale wanaopenda kukusapoti gharama kiasi kwa hii semina watutumie kwa namba hiyohiyo.

    Naomba pia kutusaidia kushare hizi taarifa kwa magroup yetu na sehemu mbalimbali ili ziwafikie walengwa mapema.Pia tunaomba waandishi wa habari watusaidie kuwajuza wananchi kwani hii ni kwa nchi nzima. Nawashukuru sana kwa Ushirikiano wenu mungu awabariki sana.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: KUBWA KULIKO:Ivo Mapunda Sports Centre imekuja na jambo jipya na jema kwako Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top