728x90 AdSpace

  • Latest News

    Saturday, June 17, 2017

    Wageni ligi kuu England wavunja rekodi yao ya usajili


    London,England.

    TIMU ya Brighton & Hove Albion ambayo imepanda daraja la ligi kuu ya soka nchini England imevunja rekodi yake ya usajili baada ya jana Ijumaa usiku kumsajili kipa namba mbili wa Valencia ya Hispania,Mathew Ryan.

    Ryan mwenye umri wa miaka 25 amejiunga na Brighton & Hove Albion kwa mkataba wa miaka mitano kwa ada ya £5m na kuwa mchezaji ghali zaidi kuwahi kusajiliwa na timu hiyo.

    Awali rekodi ya mchezaji ghali zaidi Brighton & Hove Albion ilikuwa ikishikiliwa na Shane Duffy aliyesajiliwa kwa dau la £4m mwaka 2016 akitokea Blackburn Rovers.

    Brighton & Hove Albion imeamua kumsajili Ryan baada ya kipa wake namba moja David Stockdale kudengua kusaini mkataba mpya na kuamua kujiunga na timu ya Birmingham City inayoshiriki ligi daraja la kwanza.

    Ryan alijiunga na Valencia mwaka 2015 kwa mkataba wa miaka mitano akitokea timu ya Club Brugge ya nchini Ubelgiji lakini alijikuta akiwa katika wakati mgumu baada ya kushindwa kupata namba ya kudumu kwenye kikosi cha kwanza cha miamba hiyo ya Hispania.

    Mwezi Januari mwaka huu Ryan anayeidakia pia timu ya taifa ya Australia alitolewa kwa mkopo kwenda KRC Genk inayochezewa na Mtanzania,Mbwana Samatta baada ya kuichezea Valencia mechi 10 pekee.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Wageni ligi kuu England wavunja rekodi yao ya usajili Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top