Kigali,Rwanda.
MSHAMBULIAJI hatari wa Police FC na timu ya taifa ya Rwanda,Danny Usengimana ameibuka mfungaji bora kwa msimu wa 2016/17 kwenye ligi kuu ya soka nchini Rwanda baada ya kufunga mabao 19.
Usengimana anayetarajiwa kujiunga na Singida FC kwa dau la US$100,000 (Sawa na Shilingi Milioni 82.6 za Rwanda) mara baada ya mchezo wa fainali ya kombe la Amani (Peace Cup) utakaochezwa Julai 4,amekuwa hashikiki kwenye ufungaji wa mabao tangu kuanza kwa mwaka mpya wa 2017.
Msimu uliopita Usengimana mwenye umri wa miaka 21 aliibuka tena mfungaji bora baada ya kufunga mabao 16 sawa na mshambuliaji wa zamani wa Mukura,Muhadjiri Hakizimana ambaye kwasasa anaichezea APR.
Orodha ya wafungaji bora Rwanda msimu wa 2016/17
1. Danny Usengimana (Police
FC)-19
2. Wai Yeka (Musanze FC)-18
3. Justin Mico (Police FC)-15
4. Salita Kambale (Etincelles
FC)-14
5. Shassir Nahimana (Rayon
Sport)-13
6. Shaban Hussein (Amagaju
FC)-12
7. Rashid Mutebi (Gicumbi FC)-11
8. Faruk Ssentongo (Bugesera)-11
9. Pierrot Kwizera (Rayon
Sport)-11
10. Moussa Camara (Rayon
Sports)-10
Ligi kuu ya soka nchini Rwanda imeisha wiki hii ambapo klabu ya Rayon Sports imeibuka bingwa baada ya kumaliza ikiwa na pointi 73.Ikiwa imeshinda michezo 22 imetoka sare michezo 7.Ikifungwa mchezo mmoja katika michezo 30.
0 comments:
Post a Comment